| WELCOME TO MEX DEL MOTTO
Mex09.INC. Powered by Blogger.

Translate

Monday, 30 October 2017

Masimamizi wa mitihani ya kidato cha nne wapewa onyo kali 

KATIBU MTENDAJI WA BARAZA HILO, DK. CHARLES MSONDE.

WAKATI watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kuanza mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka huu leo, Baraza la Mitihani (Necta) limetoa onyo kali
kwa wasimamizi wa mtihani huo. 


Necta imesema haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya wasimamizi hao wa mitihani pale udanganyifu wa aina yoyote utakapotokea. 

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Charles Msonde, alitoa onyo hilo jana, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtihani huo ambao watahiniwa wa shule wanatarajiwa kuwa 323,513 na wa kujitegemea 62,425. 

Dk. Msonde aliwataka wasimamizi wa mtihani huo kufanya kazi yao kwa uaminifu, uadilifu na kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwa kuwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua. 

"Udanganyifu umepungua," Dk. Msonde alisema, "mwaka 2011 watahiniwa waliofutiwa mitihani walikuwa ni 9,739, mwaka jana walikuwa 500." 

"Watahiniwa hao walibainika kufanya udanganyifu kwa kuingia na simu, vitabu na notisi kwenye vyumba vya mitihani. 
"Mwaka huu walikuwa ni watahiniwa 10 waliofanya hivyo. Hii ni dalili nzuri kuwa wanafunzi wanajiandaa vizuri." 

0 comments:

Post a Comment